1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Rais wa Iran Ahmadnejad alaumu siasa ya Marekani nchini Lebanon

14 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDLo

Rais Mamoud Ahmadnejad ameilaumu Marekani kwa kuinga mkono Israel bila ya kufikiria na pia amemlaumu rais George Bush kwa kujaribu kutatua kila jambo kwa kutumia mabomu.

Rais Ahmadnejad amesema hayo katika mahojiano ya televisheni.

Juu ya vita baina ya Israel na Hezbollah, kiongozi huyo wa Iran amesema sera ya Marekani juu ya kuinga mkono Israel inahatarisha usalama wa watu wote pamoja na wa Marekani na Ulaya.