WASHINGTON:Rais Bush amuonya kiongozi wa Iraq dhidi ya kuwa mwandani wa Iran
10 Agosti 2007Matangazo
Rais wa Marekani George Bush anamuonya Wazir MKuu wa Iraq Nuri al MALIKI dhidi ya kuwa na uhusiano wa karibu na Iran.Hii inatokea baada ya Kiongozi huyio wa Iraq kukutana na mwenzake wa Iran na kuahidi kushirikiana ili kudumisha amani na usalama nchini Iraq.
Bwana Maliki alikuwa katika ziara ya siku mbili mjini Tehran.Kauli ya Rais Bush inatokea siku kadhaa baada ya Rais wa Afghanistan Hamid Karzai kutoafutiana naye kuhusu ushawishi wa Iran katika suala la kupambana na ugaidi.Rais Karzai alikuwa ziarani Marekani wiki iliyopita.