1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Pakistan ina tanuru jipya la nyuklia ?

25 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG4O

Taasisi ya Marekani ya uchunguzi wa nyuklia imechapisha picha zinazoonesha tunuru jipya la nyuklia nchini Pakistan.

Taasisi hiyo imesema kuwa tanuru hilo linaweza kuzalisha madini ya plutonium ya kutosha ili kuunda silaha za nyuklia kati ya 40 hadi 50 kila mwaka.

Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan imekataa kusemama chochote juu ya madai hayo.

Lakini wadadisi wa masuala ya kimataifa wanaamini kuwa mradi huo mpya ni jibu la Pakistan juu ya makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni baina ya Marekani na India kuhusu kushirikiana katika matumizi ya tekinolojia ya nyuklia kwa madhumuni ya amani. Pakistan haikufurahishwa juu ya makubaliano hayo.