WASHINGTON.Marekani yataka Syria iondoshe majeshi Lebanon
7 Machi 2005Matangazo
Marekani imesema kwamba ahadi iliyotolewa na Syria juu ya kuyahamisha majeshi yake nchini Lebanon haitoshi.
Marekani imesema hayo kufuatia tangazo la rais wa Syria bwana Bashar al Assad kwamba majeshi ya nchi yake yatahamishiwa kwenye mpaka baina ya nchi yake na Lebanon.Hatahivyo rais Assad hakufafanua juu ya ratiba ya kundolewa kwa majeshi hayo.
Marekani inaitaka Syria iondoshe majeshi yake yote haraka kutoka Lebanon.
Syria ina askari alfu 15 nchini humo.