WASHINGTON:Korea ya kaskazini yafunga kinu chake kikuu cha nyuklia
15 Julai 2007Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema imeambiwa na Korea ya kaskazini kuwa nchi hiyo imekifunga kinu chake kikuu cha nyuklia cha Yongbyon ikiwa ni sehemu ya mapatano ya kupunguza silaha.
Habari hizo zimefahamika muda mfupi baada ya kuwasili ,wakaguzi kumi, wa shirika la Umoja wa Mataifa la udhibiti wa matumizi ya nishati ya nyuklia.
Wakaguzi hao wamerejea nchini Korea ya kaskazini baada ya miaka minne ili kuthibitisha utekelezaji wa hatua ya kukifunga kituo hicho .
Kutokana hatua hiyo korea ya kaskazini haitaweza kuzalisha madini ya kuundia silaha za nyuklia. Juu ya hatua ya Korea ya kaskazini mjumbe wa Marekani bwana Christopher Hill amesema uamuzi huo ni hatua ya kuelekea kwenye hatima ya kuacha kabisa mipango ya nyuklia.