WASHINGTON: Wolfowitz ahimiza pesa za wizi zirejeshwe zilikoibiwa
28 Septemba 2005Matangazo
Kiongozi wa benki kuu ya dunia Paul Wolfowitz ametaka fedha zilizoibiwa na dikteta wa zamani Sani Abacha zirejeshwe kwenye nchi zilikoibwa.
Wolfowitz amekuwa kwenye mstari wa mbele katika juhdi za Nigeria za kutaka kurejeshwa kiasi cha dola milioni 458 zilizowekwa kwenye akaunti za benki ya uswisi na Sani Abacha aliyefariki mwaka 1998.
Uswisi imekubali kuzitoa pesa hizo.Uswisi ilisisimamisha akaunti hizo mwaka 1999 lakini ilikataa kuzirejesha kwa nchi husika kwa madai kwamba inataka kupata hakikisho juu ya jinsi pesa hizo zitakavyotumiwa.
Uamuzi wa Wolfowitz umetokana na kile alichokiita kuvutiwa na hatua za rais Obasanjo wa Nigeria za kupambana na rushwa, kuimarisha uwazi na kutekeleza mageuzi ya kiuchumi nchini humo.