Washington. Waziri mkuu wa Japan azuru Marekani.
27 Aprili 2007Rais wa Marekani George W. Bush amemkaribisha waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe katika Ikulu ya Marekani.
Ni ziara ya kwanza rasmi ya waziri mkuu Abe nchini Marekani tangu kuchukua wadhifa huo.
Aliandaliwa chakula cha jioni ambacho kilikuwa mfano wa chakula cha wanafamilia kwa heshima yake.
Leo Ijumaa , viongozi hao wawili wanatarajiwa kuwa na mazungumzo rasmi katika mahali anapopumzikia rais huko Camp David , Maryland.
Majadiliano kuhusu Korea ya kaskazini , Iraq na Afghanistan yanatarajiwa kuwa juu katika ajenda za mkutano huo. Ziara ya Abe inaonekana kuwa ni shukrani kutoka kwa rais Bush kwa mchango wa Japan kwa ajili ya juhudi za kivita nchini Iraq na Afghanistan.