WASHINGTON: Washirika wa NATO wasaidie zaidi kijeshi
16 Februari 2007Matangazo
Mashambulio yakizidi kuendelea nchini Afghanistan,rais George W.Bush wa Marekani amewataka washirika wa NATO kutoa mchango zaidi. Amesema,washirika hao wanapaswa kufuata mfano wa Marekani na kuchangia wanajeshi zaidi ili kuziba pengo la usalama.Akizungumza mjini Washington, Bush alisema,zisiwepo sheria maalum za kitaifa kuhusu maeneo ya kupeleka vikosi vyake.Kuhusika na suala hilo,Ujerumani inayoweka vikosi vyake kaskazini mwa Afghanistan tu,imekosolewa mara kadhaa.Marekani inapeleka wanajeshi 3,200 wengine kujiandaa kupambana na Wataliban, ikihofiwa kuwa wanamgambo hao wataimarisha mashambulio yao pale hali baridi ya barafu itakapoanza kubadilika wakati wa majira ya machipuko.