WASHINGTON: Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu Darfur
8 Machi 2007Matangazo
Ripoti ya kila mwaka ya Marekani kuhusu haki za binadamu kote duniani inasema mauaji ya halaiki yanayoendelea katika jimbo la Darfur,magharibi mwa Sudan,ni ukiukaji mkubwa kabisa wa haki za binadamu uliotokea mwaka 2006.Ripoti ya wizara ya mambo ya nje inasema vikosi vya waasi na vya serikali ya Sudan vinaendelea kuvunja haki za binadamu na kwamba hadi mwisho wa mwaka 2006 kama watu 200,000 walipoteza maisha yao.Ripoti hiyo imechunguza nchi 190 na imegundua kuwa Venezuela, Urussi na Eritrea,ama zimefanya maendeleo madogo au hakuna kilichofanywa kutenzua matatizo ya kuvunjwa haki za binadamu.Iran,Korea ya Kaskazini na Zimbabwe ni miongoni mwa nchi zingine zilizotajwa katika ripoti hiyo.