WASHINGTON Syria yatakiwa kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Lebanon.
18 Februari 2005Matangazo
Rais George W Bush wa Marekani ameitaka Syria kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Lebanon. Amesema atatafuta kuungwa mkono na viongozi wa mataifa ya Ulaya kuishinikiza Syria. Katika mkutano wake na waandishi habari mjini Washington, rais Bush alisema Syria ni kikwazo kikubwa kwa juhudi za kupatikana amani katika mashariki ya kati. Syria imekabiliwa na shinikizo kubwa la kimataifa tangu mauji ya waziri mkuu wa zamani Rafik Hariri Jumatatu iliyopita. Raia wa Lebanon wanailaumu serikali ya Damascus kwa kuhusika na mauaji hayo.