1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Raia wa Marekani nchini Kenya na Ethiopia watahadharishwa

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwX

Marekani imetahadharisha raia wake hapo jana kwamba Kenya na Ethiopia zinaweza kukabiliwa na mashambulizi ya kujitolea muhanga maisha ya watu wa itikadi kali kutoka Somalia ambapo Muungano wa Mahkama za Kiislam unadhibiti mji mkuu wa nchi hiyo pamoja na maeneo mengine.

Ujumbe uliotolewa kwa raia wa Marekani na balozi za Marekani nchini Kenya na Ethiopia umesema vitisho hivyo hususan vimetaja uripuaji wa mabomu wa kujitolea muhanga maisha katika maeneo mashuhuri nchini Kenya na Ethiopia.

Raia hao wa Marekani wametakiwa kuwa waangalifu sana wakati wanapotembelea maeneo mashuhuri nchini Kenya,Ethiopia na katika nchi za jirani ambazo hazikutajwa jina.

Onyo hilo inasemekana limetolewa kutokana na taarifa katika tovuti za Somalia zinazodhaniwa kutoka kwa Sheikh Hassan Dahir Aweys ambaye ni kiongozi mkuu wa Waislamu wa msimamo mkali nchini Somalia ambaye ameridhia operesheni za kujitolea muhanga maisha.

Hata hivyo msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Marekani Sean McCormack amekataa kutowa ufafanuzi mahsusi wa tishio hilo.