WASHINGTON: Mazungumzo ya simu na barua pepe kudakwa Marekani
5 Agosti 2007Matangazo
Bunge la Marekani,limeidhinisha mswada wa sheria itakayoruhusu mashirika ya upelelezi ya Marekani, kudaka mazungumzo katika simu za kimataifa na hata barua pepe,bila ya hapo kabla kuomba ruhusa ya jaji.Mswada huo,hapo awali,uliidhinishwa na Seneti.
Mashirika yanayotetea uhuru wa kiraia yamesema,hatua hiyo imevuka mno mipaka.Mwanzoni sheria hiyo,itaruhusiwa kutumika kwa kipindi cha miezi sita.Rais George W.Bush wa Marekani amesema hatua hiyo inahitajiwa kupambana na vitisho vya kigaidi.