1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington: Marekani yawapiga marufuku wapinzani wa Lebanon.

30 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBn9

Maafisa wa serikali ya Marekani wamesema watawapiga marufuku ya kuingia nchini Marekani watu wote wanaotuhumiwa kwamba wanaitatiza serikali ya Lebanon.

Orodha hiyo inajumuisha wanasiasa, maafisa wa serikali pamoja na wafanyi biashara kutoka Lebanon na Syria.

Hatua hiyo inawalenga wapinzani wa taasisi za serikali ya Lebanon inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.

Marekani imekuwa ikiishutumu Syria kwa kuingilia maswala ya ndani ya Lebanon na pia inaituhumu kwa kuunga mkono vyama vya Hizbullah na Hamas.