1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yaidhinisha fedha za kugharamia vita Iraq

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByC

Rais George W Bush wa Marekani ametia saini mswada unaoidhinisha dola bilioni mia moja za kugharamia vita vya Iraq.

Hatua hiyo imemaliza mzozo ulioendelea kwa muda wa miezi minne kati ya Rais George Bush na bunge la Congress lenye wabunge wengi wa chama cha Demokratic waliokuwa wamependekeza muda wa kuyaondoa majeshi ya Marekani nchini Iraq utangazwe.

Wakati huo huo maafisa wa Iraq na Uingereza wamesema vikosi maalum vya Iraq vimempiga risasi na kumuua Wissam Abu Qader, kamanda wa wanamgambo wa kundi la Mahdi linaoongozwa na kiongozi wa Kishia Moqtada al-Sadr.

Saa chache baadaye, Moqtada Sadr, ambaye amekuwa mafichoni tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita, alijitokeza hadharani katika msikiti wa Kufa.

Kiongozi huyo wa kishia amerejea wito wake kwamba wanajeshi wa Marekani waondoke nchini Iraq.