WASHINGTON. Marekani kufanya juhudi za kusimamisha mapigano Lebanon
31 Julai 2006Waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice amesema Marekani itafanya juhudi ili umoja wa mataifa upitishe azimio juu ya kusimamisha mapigano nchini Lebanon.
Bibi Rice amesema hayo baada mazungumzo yake na waziri m kuu wa Israel bwana Ehud Olmert.
Kauli ya bibi Rice inafuatia mashambulio makubwa yaliyofanywa na ndege za Israel katika mji wa Qana ambapo raia zaidi ya sitini waliuwawa katika nyumba waliyokuwa wamejificha.
Juu ya ulazima wa kuafikiwa hatua ya kusimamisha mapigano mara moja nchini Lebanon waziri wa mambo ya nje wa Marekani amesema.
Oton…Nina hakika mnamo wiki hii tutafikia hatua hiyo. Kwani ni kufikia hatua hiyo tu kwamba irtawezekana kwa watu wa Lebanon kuudhibitri mustakbaal wa nchi yao na pia watu wa Israel wataweza kuepuka mashambulio yanayofanywa na makundi ya kigaidi ya nchini Lebanon.
Wakati huo huo Israel imesimamisha mashambulio yake huko kusini mwa Lebanon kufuatia shambulio la jana katika mji wa Qana ambalo wengi waliouwawa walikuwa ni watoto.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limelaani mauaji hayo lakini wakati huo huo limeshindwa kuunga mkono mwito wa katibu mkuu Kofi Annan unaotaka mapigano hayo yasimamishwe mara moja.