1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Marekani imejifunga na mabadliko ya hali ya hewa

27 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBM8

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice leo amefunguwa mkutano wa nchi 16 zinazotowa kwa wingi gesi yenye kuathiri mazingira duniani kwa kuahidi Marekani inachukulia kwa uzito tishio la kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.

Rice ameuliza mwanzoni mwa mkutan huo ni dunia ya aina gani wanaotaka kuishi na ni dunia ya aina gani wanayotaka kuikabidhi kwa kizazi kijacho.

Amesema Marekani inalichukulia suala mabadiliko ya hali ya hewa kwa makini kwa kuwa ni taifa kubwa la kiuchumi na pia ni mtowaji mkubwa wa gesi zenye kuathiri mazingira duniani.

Nchi hizo zinatazamiwa kuandaa malengo ya kupunguza utowaji wao wa gesi zenye kuathiri mazingira na kuoanisha nguvu za makampuni na teknlojia mpya katika kupambana na uchafuzi huo wa mazingira.