1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Kutolewa picha za Saddam kwachunguzwa

21 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFBf

Jeshi la Marekani linachunguza vipi picha za Saddam Hussein akiwa gerezani zimeyafikia majarida mjini New York na London wakati gazeti la Uingerezea likitowa picha nyengine mpya ya dikteta huyo wa zamani huku kukiwa na shutuma kwamba hatua hiyo yumkini ikawa inakiuka Makubaliano ya Geneva.

Gazeti la Sun ambalo picha zake za awali zimepelekea uchunguzi wa duru zake limechapisha picha nyengine zaidi ya Saddam leo hii iliopigwa juu ya senyenyenge akionekana kutembea na kama anazungumza na mtu.

Picha nyengine tafauti zimemuonyesha binamu wa Saddam Ali Hassan al Majid ambaye anajulikana kwa jina la Kemikali Ali kutokana na dhima aliyotimiza katika mashambulizi ya kutumia gesi kaskazini mwa Iraq dhidi ya Wakurdi hapo mwaka 1987 na mtalaamu wa biolojia Huda Salih Mahdi Ammash aliyepachikwa jina la Bibi. Anthrax na Kemikali Sally kwa madai ya kuhusika katika mpango wa Saddam wa silaha za maangamizi.

Katika toleo lake la jana asubuhi gazeti hilo lilichapisha kwenye ukurasa wake wa mbele picha ya Saddam akiwa na suruali ya ndani tu ikiandamana na kichwa cha habari Dhalimu likiwa na kichupi.

Kutokana na kuchapishwa kwa picha hizo mawakili wa Saddam wamesema wanafikiria kuchukuwa hatua ya kisheria dhidi ya gazeti hilo.