1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Kansela Schröder ziarani Marekani

28 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEzK

Kansela Gehard Schröder wa Ujerumani kwa mara nyingine amesisitiza dhamira ya nchi yake ya kuwa na kiti cha kudumu kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Bwana Schröder amesisitiza hayo kwenye mkutano wake na rais G.Bush wa Marekani.

Kiongozi huyo wa Ujerumani anayefanya ziara nchini Marekani amesema kwamba nchi yake inashiriki katika kutekeleza majukumu ya kimataifa katika sehemu zenye mizozo duniani. Na ndiyo sababu kwamba nchi yake ina haki ya kuwa katika mstari wa mbele inapobidi kupitisha maamuzi muhimu.

Rais Bush ameeleza kwamba hapingi ombi hilo la Ujerumani lakini haliungi mkono.

Kansela Schröder na mwenyeji wake pia walizungumzia juu ya masuala ya matokeo ya uchaguzi nchini Iran,hali ya nchini Irak na mgogoro wa Umoja wa Ulaya.

.