1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Italia na Marekani zinatofautiana kuhusu mauaji ya Calipari

30 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFI2

Marekani na Italia zimesema hazikubaliani na hitimisho la uchunguzi wa pamoja uliofanywa kuhusu mauaji ya ajenti wa Kitaliana nchini Iraq.Nicola Calipari alipoteza maisha yake alipojaribu kumkinga mateka wa Kitaliana,baada ya gari lao kufyetuliwa risasi na wanajeshi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.Ripoti zasema,kwa maoni ya wachunguzi wa Kimarekani,wanajeshi hao hawana makosa.Waziri wa mambo ya kigeni wa Italia,Gianfranco Fini amesema,Italia itaendelea kufanya uchunguzi mwingine kuhusu kifo cha Calipari.Kwa wakati huo huo,taarifa ya pamoja iliyotolewa na Marekani na Italia imesema,licha ya tukio hilo,nchi hizo mbili ni washirika imara.