1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington: Israel yaionya Marekani kuhusu nyuklia

13 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEDy
Waziri wa ulinzi wa Israel Shaul Mofaz anayezuru Marekani, alisema ameelezea wasiwasi wa nchi ykae kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran, katika mazungumzo yake pamoja na maafisa wa Marekani na aliahidi kwamba serikali yake itaunga mkono kile kinachoitwa "ramani" ya safari ya amani pamoja na Wapalestina. "Tulizungumza juu ya Iran, Iraq na Wapalestina, hasa hasa kuhusu serikali ya Abu Ala, ambayo imeidhinishwa hii leo na bunge la Palsestina," alisema akimaanisha baraza jipya la mawaziri la Waziri Mkuu Ahmed Qorei. Afisa wa Israel alisema hapo awali, kwamba Mofaz alilizusha suala la Iran pia katika mazungumzo yake na waziri wa ulinzi Donald Rumsfel jumanne, sawa na wasiwasi wa Israel kuhusu kuendelea Syria kuunga mkono vikundi dhidi ya Israel kama Hamas na Islamic Jihad.