1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON Dereva wa zamani wa Osama bin Laden kujibu mashtaka

16 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEuA

Mahakama moja nchini Marekani imeamua kwamba mtu anayesemekana alikuwa mlinzi wa Osama bin Laden anaweza kujibu mashtaka mbele ya tume maalumu ya jeshi.

Salim Ahmed Hamdan ni mfungwa katika jela ya Guantanamo Bay nchini Cuba na anakabiliwa na mashtaka ya kuwa na njama ya kuwashambulia raia, mauaji, kuharibu mali na ugaidi. Waongoza mashataka katika tume hiyo ya jeshi wamesema bwana huyo alikuwa dereva wa kiongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, Osama bin Laden katika miaka ya mwisho ya 1990.

Jaji alisimamisha kusikilizwa kwa kesi ya Hamdan mwezi Novemba mwaka jana akisema haingeweza kuendelea mpaka wakati itakapobainika ikiwa alikuwa mfungwa katika jela ya Guantano kwa mujibu wa mkataba wa Geneva. Serikali ya rais George W Bush imekuwa ikisisitiza kwamba mkataba huo wa Geneva hauwezi kutumiwa katika kesi za wafungwa wa jela ya Guantanamo.