1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush asaini sheria ya bajeti ya jeshi ya mwaka wa 2004-

25 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFy9

Rais George W Bush wa Marekani, amesaini sheria inayoongeza bajeti ya matumizi ya jeshi la Marekani mwaka ujao wa 2004, kwa zaidi ya asilimia mbili; kulingana na bajeti ya jeshi hilo mwaka huu wa 2003.

Kulingana na waraka huo, jeshi la Marekani litakua na kitita cha dola biliyoni mianne na moja.

Katika sherehe iliyoambatana na kusainiwa sheria hio, iliyofanyika katika wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, Rais George W Bush amesema serikali yake itaendelea kufanya kila iwezalo, ili Marekani iendelee kua dola lenye nguvu, kuhakikisha usalama wa raia wake, na amani katika sehemu nyingine za dunia.

Jana, Rais George W Bush alikua na mazungumzo na familia za wanajeshi 31 wa kimarekani, waliofariki nchini Irak; wa kambi ya kijeshi ya FORT CARSON- Colorado, magharibi mwa Marekani.

Wanajeshi elfu moja miambili wa kambi hio, walipelekwa kushiriki katika operesheni za jeshi la Marekani nchini Irak.