WASHINGTON: Bush ameahidi msaada wa pesa
9 Septemba 2005Matangazo
Rais George W.Bush wa Marekani ametoa ahadi kwa watu walionusurika na kimbunga Katrina kuwa moja kwa moja kila familia itapewa msaada wa Dola 2,000.Vile vile amesema familia zilizohamishwa kwengine zitaendelea kupokea msaada wa matibabu.Kwa wakati huo huo Baraza la Congress limeidhinisha msaada mwengine wa dharura wa Dola bilioni 51.8 kama ilivyoombwa na serikali.Na katika eneo la mafuriko la New Orleans,polisi na wanajeshi wanasaka kila nyumba kwa lengo la kuwahamisha wakaazi wote.Inasemekana kuwa maji ya mafuriko yaliochafuka ni kitisho kikubwa kwa afya.Hadi hivi sasa watu 5 wameshafariki kwa sababu ya maambukizo yaliotokana na maji yaliyochafuka.Kuna khofu kuwa elfu kadhaa ya watu wamefariki katika kimbunga Katrina.