1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON :Annan asema Marekani ishirikiane na wengine

12 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCk2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anaeondoka madarakani ametoa mwito kwa Marekani kuachana na diplomasia ya kuchukua hatua peke yake na amesema haki za binadamu pia ziheshimiwe wakati wa kupambana na ugaidi.Akizungumza Missouri nchini Marekani,Annan alisema jumuiya za kimataifa zitafanikiwa zaidi ikiwa Marekani itashirikiana nazo.Akamnukulu rais wa zamani wa Marekani Harry Truman aliesema,wajibu wa madola makuu ni kuhudumia na sio kutawala binadamu duniani.Annan,mara kwa mara amepambana na serikali ya rais George W.Bush,hasa kuhusika na uvamizi wa Irak wa mwaka 2003.Annan vile vile ametoa mwito wa kuchukua hatua kuhusu mgogoro wa Darfur,magharibi ya Sudan,licha ya upinzani wa Khartoum.Ban Ki-Moon wa Korea ya Kusini anamrithi Katibu Mkuu Kofi Annan anaeondoka Umoja wa Mataifa Desemba 31 baada ya kushika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 10.