WARSAW:Serikali ya mseto mashakani baada ya kufutwa kazi naibu waziri mkuu
10 Julai 2007Matangazo
Serikali ya mseto nchini Poland inaelekea kutumbukia kwenye mzozo baada ya waziri mkuu Jaroslaw Kaczynski kumfuta kazi naibu wake Andrzej Lepper.
Hatua hiyo ya waziri mkuu inatishia mustakaba wa serikali ya mseto ambayo tayari inawingi mdogo bungeni.
Andrzej amefutwa kazi baada ya kuhusishwa kwenye kesi kubwa ya rushwa lakini amekanusha madai hayo.
Waziri mkuu amewaambia waandishi wa habari kwamba hali hiyo ya mashaka huenda ikasababisha uchaguzi wa mapema lakini chama cha upinzani cha mrengo wa kushoto kimesema kitawasilisha hoja ya kufanyika kura ya kutokuwa na imani na serikali.