1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WARSAW:Rais Köhler wa Ujerumani awasili Poland kwa ziara ya siku tatu.

30 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEg9

Rais wa Ujerumani,Horst Köhler amewasili mjini Warsaw akianza ziara rasmi ya siku tatu nchini Poland.RaisKöhler alilakiwa na mwenyeji wake,rais wa Poland,Alexander Kwasniewski.

Ziara hiyo ya Rais Köhler imekwenda sambamba na siku ya kuadhimisha miaka 25 tangu kuzaliwa kwa chama cha Solidarty Labour Movement.Pia ziara hiyo inakwenda sawia na maadhimishao ya miaka 66 tangu Manazi wa Kijerumani walipoivamia Poland.

Rais Köhler ataweka mashada ya maua katika kaburi la askari asiyefahamika na katika mnara wa Warsaw wa kumbukumbu wa harakati za kudai haki.Pia ataweka jiwe la msingi katika sehemu itakayojengwa ubalozi mpya Ujerumani mjini Warsaw.