WARSAW: Ziara ya Merkel kurekebisha uhusiano
17 Machi 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anaendelea na ziara yake ya siku mbili nchini Poland,yenye azma ya kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Masuala ya utata ni sera za nishati na usalama kuhusika na Urussi na vile vile katiba ya Umoja wa Ulaya.Merkel ambae hivi sasa ameshika wadhifa wa urais katika Umoja wa Ulaya,ameahidi kupata maafikiano ili viongozi wa umoja huo waweze kuendelea na kazi za kukamilisha mkataba huo watakapokutana mwezi Juni,na hivyo Katiba ya Umoja wa Ulaya ipate kuidhinishwa ifikapo mwaka 2009.Kansela Merkel vile vile amesema,suala lililozusha mabishano kuhusika na mradi wa Marekani kutaka kuweka makombora ya kujikinga nchini Poland,lazima lipatiwe ufumbuzi katika Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi-NATO.