WARSAW : Wapoland wambwaga Waziri Mkuu Kaczynski
22 Oktoba 2007Wapiga kura nchini Poland wamemgeukia waziri mkuu Jaruslaw Kazynski na kuupa upinzani wa mrengo wa kulia wa wastani ushindi mkubwa.
Baada ya theluthi tatu ya kura kuhesabiwa chama cha Civic Platform cha Sera za kiraia kimejipatia asilimia 41 ya kura.Chama cha Waziri Mkuu Kaczynski cha Sheria na Haki kimeshindwa kwa kujipatia asilimia 32 tu ya viti.Kiongozi wa chama Sera za Kiraia Donald Tusk kampeni yake imelenga kwenye kutetea sera za biashara na kuunga mkono Umoja wa Ulaya kinyume na msimamo wa Kaczynski wa kuvuruga mambo ndani ya Umoja wa Ulaya.
Chama mshirika kinachoweza kujumuishwa kwenye serikali ya mseto yumkini kikawa ni chama cha msimamo wa wastani cha Wakulima.
Uchaguzi wa hapo jana umevutia umma mkubwa wa wapiga kura nchini Poland kuwahi kushuhudiwa tokea kuanguka kwa utawala wa Kikomunisti.