WARSAW: wapinzani washinda uchaguzi nchini Poland
22 Oktoba 2007Matangazo
Chama cha upinzani kimeshinda uchaguzi wa bunge nchini Poland. Waziri mkuu wa hadi sasa Jaroslaw Kaczynski wa chama cha kihafidhina amekubali kushindwa .
Chama cha upinzani kinatetea hoja ya kusawazisha uhusiano na nchi za Umoja wa Ulaya na kuharakisha mageuzi ya uchumi.
Chama hicho kimeshinda kwa kupata karibu asilimia 40 ya kura.
Wananchi wengi wa Poland walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo uliofanyika jana.