WARSAW : Uchaguzi wa Rais Poland kurudiwa
10 Oktoba 2005Katika uchaguzi wa Rais nchini Poland uliofanyika hapo jana mbunge anayetetea uchumi unaotegemea nguvu za soko Donald Tusk ameweza kuongoza kwa kura chache dhidi ya Meya wa mji wa Warsaw Lech Kaczynski.
Maafisa wa uchaguzi wanasema wakati zaidi ya asilimia 90 ya kura zikiwa zimehesabiwa asilimia 35.8 zimekwenda kwa Tusk wakati asilimia 33.3 wamempigia kura Kaczynski.Matokeo hayo yanawalazimisha wanaharakati hao wa zamani wa chama cha Solidarity cha kupiga vita ukomunisti kupambana tena katika marudio ya uchaguzi hapo tarehe 23 mwezi huu wa Oktoba.
Tusk anataka kuuchochea uchumi kwa kuweka kodi ndogo na kundowa urasimu ili kuongeza ajira wakati Kaczynski amekuwa akipiga kampeni ya kuwa na mtandao madhubuti wa usalama wa jamii.