WARSAW: Rais Kaczynski atoka hospitalini
3 Septemba 2007Matangazo
Rais wa Poland, Lech Kaczynski, amerejea nyumbani kwake baada ya kulazwa kwa muda mfupi katika hospitali ya jeshi mapema leo kufuatia homa kali na maumivu ya tumbo.
Msemaji wa hospitali ya jeshi alikolazwa rais Kaczynski amesema kiongozi huyo hayuko katika hali mbaya kiafya na akaongeza kuwa atarudi kazini na kuendelea na majukumu yake kama kawaida.
Vyombo vya habari nchini Poland vimekuwa vikizungumzia wasiwasi uliopo kuhusu hali ya afya ya rais Kaczynski ambayo imemlazimu kiongozi huyo kushindwa kukamilisha majuku yake rasmi.
Lakini ofisi ya rais mjini Warsaw imekuwa mara kwa mara ikikanusha kwamba rais Kaczynski ana matatizo makubwa kiafya.