Warsaw. Poland yaahidi kupeleka wanajeshi katika jeshi la NATO Afghanistan.
15 Septemba 2006Poland imetangaza kuwa itatuma kikosi cha wanajeshi 1,000 nchini Afghanistan kama sehemu ya jeshi la kulinda amani la NATO nchini humo.
Hii inakuja baada ya makamanda wa jeshi la NATO kuomba wanajeshi wa ziada 2,500 kutoka mataifa wanachama wa NATO ili kuharakisha mapambano dhidi ya wapiganaji wa Taliban.
Jeshi la Poland linatarajiwa kuwasili mwezi wa Februari.
Wakati huo huo Ukraine imeiambia NATO kuwa inasitisha mpango wake wa kujiunga na jeshi hilo la kujihami la mataifa ya magharibi.
Akizuru makao makuu ya NATO mjini Brussels , waziri mkuu Viktor Yanukovich amesema kuwa muda wa kupumzika unahitajika kwasababu ya upinzani wa theluthi tatu ya wananchi wa Ukraine. Yanukovich hata hivyo amesisitiza kuwa Ukraine inataka kujiunga na umoja wa Ulaya.