WARSAW. Poland nayo yaahirisha kura ya maoni juu ya umoja wa ulaya
22 Juni 2005Rais Aleksander Kwasniewski wa Poland ametangaza kuahirishwa kwa kura ya maoni juu ya katiba ya umoja wa ulaya kwa muda usio julikana.
Rais Aleksander aliwahutubia waandishi wa habari mjini Warsaw na akasisitiza kuwa kura hiyo ya maoni imeahirishwa na wala sio kufutiliwa mbali na kwamba itafanyika baadae.
Poland ilitarajiwa kupiga kura ya maoni juu ya katiba ya umoja wa ulaya mwezi oktoba.
Alisema kuwa kuendelea na mpango kutekeleza kura hiyo si jambo muafaka hasa baada ya katiba ya ulaya kukataliwa na nchi mbili wanachama.
Poland imeandaa mkutano na mawaziri wa mambo ya nje wa umoja wa ulaya kutoka Ufaransa na Ujerumani wiki ijayo mjini Warsaw.
Rais Aleksandar alifikia uamuzi huo baada ya kushuriana na waziri wake mkuu Marek Belka na spika wa bunge la Poland Wlodzimierz Cimoszewicz.