1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WARSAW : Misa ya kumthibistiha Askofu yafutwa

7 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcb

Misa ya Jumapili iliokuwa imepangwa kumthibitsiha Askofu Mkuu mpya wa Warsaw leo hii imefutwa.

Kufuatia juma zima la hali ya mashaka Askofu Mkuu Stanislaw Wielgus amekiri kushirikiana na majasusi wa enzi ya ukomunisti nchini Poland lakini amekanusha kutowa habari juu ya makasisi.Suala hilo limekuwa chanzo cha tahayuri kwa Kanisa.

Kanisa Katoliki la Poland lilitimiza dhima muhimu katika kuupinga ukomunisti nchini humo ambao ulikuja kusambaratika hapo mwaka 1989.

Lakini wanahistoria wanaamini kwamba hadi asilimia 10 ya makasisi yumkini wakawa wametowa ushirikiano wao kwa maafisa wa serikali ya kikomunisti.