Warsaw. Mhafidhina adai kupata ushindi katika uchaguzi.
24 Oktoba 2005Mgombea wa kiti cha urais kutoka katika chama cha kihafidhina Lech Kaczynski amedai kuwa ameshinda uchaguzi wa pili nchini Poland.
Maafisa wa tume ya uchaguzi wanasema kuwa meya huyo wa zamani wa mji wa Warsaw , Kaczynski anaongoza kwa kiasi cha asilimia 10 dhidi ya mpinzani wake Donald Tusk huku kura nyingi zikiwa zimekwisha hesabiwa.
Tusk ambaye ameahidi kuupsukuma mbele uchumi wa Poland , amejikuta uongozi wake ukipungua kwa kiwango kikubwa dhidi ya Kaczynski katika siku za mwisho za kampeni ya uchaguzi.
Kaczynski amepata kuungwa mkono zaidi kwa ahadi za kulinda mfumo wa misaada ya kijamii huku kukiwa na upungufu mkubwa wa nafasi za ajira.
Wakati wa kampeni hizo , mgombea huyo kutoka chama cha kihafidhina alizungumzia juu ya kukabiliana na Russia na Ujerumani pamoja na kuwaondoa kutoka katika nyadhifa zenye nguvu wakomunist waliokuwa wakitawala zamani nchini humo.