WARSAW: Merkel amekamilisha ziara nchini Poland
17 Machi 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Poland.Msemaji wa serikali,Ulrich Wilhelm alipozungumza muda mfupi kabla ya Kansela Merkel kurejea Ujerumani, alisema ziara hiyo imekwenda vizuri.Akaongezea kuwa majadiliano kati ya Kansela Merkel na Rais wa Poland,Lech Kaczynski yameboresha msingi wa imani.Amesema huo ni msingi mzuri wa kusuluhisha matatizo ya hivi sasa.Ziara ya Merkel nchini Poland hasa ilikuwa na azma ya kuboresha uhusiano wenye mvutano,kati ya Ujerumani na Poland.Siku ya Ijumaa,alipozungumza kwenye Chuo Kikuu cha Warsaw mbele ya wanafunzi na wanataaluma,Merkel alisema ataendeleza juhudi za kujumuisha nchi za Ulaya. Wakati huo huo alisisitiza umuhimu wa kuwa na Katiba ya Ulaya.