WARSAW : Kimbuga chauwa zaidi ya 40 na hasara ni kubwa
20 Januari 2007Poland na Jamhuri ya Czech nazo zimekumbwa na kimbunga ambacho kimepiga eneo zima la kaskazini mwa Ulaya na kusababisha vifo vya takriban watu 45.
Kimbunga hicho hivi sasa kinaelekea Urusi na Ukraine. Nchi kadhaa za bara la Ulaya zilizoathiriwa na kimbunga hicho zimekuwa zikisafisha athari za kimbunga hicho ambacho kimefunga mifumo ya usafiri,kutibuwa usambazaji wa nishati na kusababisha hasara ya zaidi ya euro bilioni moja.
Watu 13 wameuwawa nchini Uingereza kutokana na ajali za kimbunga hicho,watu 11 wameuwawa nchini Ujerumani,sita nchini Uholanzi,sita nchini Poland,wanne katika Jamhuri ya Czeck, wawili wameuwawa nchini Ubelgiji na watatu nchini Ufaransa.
Mamia kwa maelfu ya nyumba katika nchi kadhaa za Ulaya zimekosa umeme wakati kimbunga hicho cha upepo mkali kilipon’gowa miti na nyaya za umeme.