Warsaw. Kansela wa Ujerumani ziarani Poland na Jamhuri ya Cheki.
17 Mei 2005Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder amekwenda katika mji mkuu wa Poland Warsaw kushiriki katika mkutano wa umoja wa Ulaya.
Viongozi kutoka mataifa 46 wako mjini Warsaw kwa mkutano wao wa siku mbili wakijadili masuala kama usafirishaji haramu wa watu, ugaidi, uhamishaji wa fedha kinyume na sheria pamoja na uhalifu wa kupangilia.
Bwana Schroeder ataendelea baada ya hapo hadi katika jamhuri ya Cheki ambako atakuwa kiongozi wa kwanza kutoka nje kukutana na kiongozi mpya wa nchi hiyo waziri mkuu Jiri Paroubek.
Kansela atatembelea maeneo ya mji wa Terezin ambako wahanga wa mauaji ya holocost yalifanyika wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia, na pia katika mji wa Teresienstadt, mji ambao Wanazi waliutumia kama kambi ya kuwaweka Wayahudi katika huo wa vita.