Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia, Matteo Salvini, ameagiza sensa kwa Waroma waishio nchini Italia, na kusema watakaogundulika kutokuwa raia wa nchi hiyo, wafukuzwe. Takribani wiki moja baada ya kauli hiyo, mtu mmoja kutoka jamii hiyo ya Waroma aliuawa katika shambulizi dhidi ya kambi yao Mashariki mwa Ukraine. Jamii ya Roma, ambayo imeishi Ulaya kwa zaidi ya miaka 1000, iko hatarini?