1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jack Warner atishia kumwaga mtama kuhusu FIFA

4 Juni 2015

Uchunguzi wa rushwa na ufisadi katika FIFA unaofanywa na shirika la upelelezi la Marekani – FBI, unajumuisha namna shirikisho hilo la kandanda lilivyotoa vibali kwa Urusi na Qatar kuandaa fainali za Kombe la Dunia

https://p.dw.com/p/1FbdK
FIFA-Funktionär Jack Warner
Picha: Luis Acosta/AFP/Getty Images

Urusi na Qatar zimekanusha kufanya makosa yoyote kuhusiana na maombi yao ya kuandaa fainali za 2018 na 2022, ambayo hayakuwa chini ya mashtaka yaliyotangazwa waendesha mashtaka wa Marekani wiki moja iliyopita dhidi ya maafisa wa FIFA ambayo yaliushangaza ulimwengu.

Hapo jana, sehemu ya nakala ya mahakama ya Novemba 2013 ambayo raia wa Marekani na mwanachama wa kamati kuu ya FIFA kuanzia 1997 hadi 2013 Chuck Hagel alikiri kuwa na hatia, ilionyesha kuwa yeye pamoja na wengine katika shirikisho hilo walikubali rushwa katika kutoa vibali vya Kombe la Dunia 1998 nchini Ufaransa na 2010 Afrika Kusini na vinyang'anyiro vingine.

Nyaraka nyingine tofauti za koti zinaonyesha madai ya mwendesha mashtaka kuwa Morocco ilitoa hongo kwa afisa mwingine wa kamati kuu ya FIFA, Jack Warner wa Trinidad and Tobago, na kuwa Blazer alitumika kama mpatanishi. Warner amekanusha hilo pamoja na tuhuma nyingine dhidi yake, na jana usiku ametoa taarifa kwenye televisheni akisema anahofia maisha yake, lakini atawaeleza wapelelezi kila kitu anachokifahamu kuhusu ufisadi katika FIFA. "Nina nyaraka nyingi zilizo na maelezo ya kutosha, ikiwa ni pamoja na hundi na taarifa zinazowiana, na nimeziweka katika mikono tofauti na yenye kuheshimika. Zinahusu ufahamu wangu na kuhusika kwangu katika uhusiano kati ya FIFA, ufadhili wake na mimi, uhusiano kati ya FIFA, ufadhili wake na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 nchini Trinidad and Tobago".

Vereinigte Arabische Emirate Chuck Blazer in Abu Dhabi
Afisa wa Zamani wa FIFA, Mmarekani Chuck Blazer akiri kupokea hongoPicha: picture alliance/dpa/A. Haider

"Qatar inaonea"

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Qatar Khaled al-Attiyah amesema nchi yake haiwezi kupokonywa kibali cha kuandaa tamasha hilo akiongeza kuwa ni Qatar inapigwa vita na watu wabaguzi "Baadhi ya mashirika, baadhi ya nchi, hazipendi kuliona taifa la Kiarabu katika Mashariki ya Kati likiandaa kiynang'anyiro kama hiki katika ulimwengu wa kiarabu. Qatar, wakati tulitangaza nia hii, hatukujiwekea mabegani mwetu tu, bali kwa eneo zima la Mashariki ya Kati"

Kwa upande wake, Urusi imepuuza wasiwasi kuwa huenda ikapoteza kibali cha kuandaa Kombe la Dunia. Msemaji wa Rais wa Urusi Vladmir PUTIN, amesema amesema wanashirikiana na FIFA na muhimu ni kuwa wanaendelea na maandalizi ya Kombe la Dunia la 2018.

FIFA imekanusha kuwa afisa wake mwingine, Karibu Mkuu Jerome Valcke, alihusika katika malipo ya dola milioni 10 kama hongo yaliyofanywa na shirikisho la kandanda la Afrika Kusini, ambayo yanachunguzwa na Marekani. Waziri wa michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula alithibitisha kumpa Warner fedha hizo wakati wa mchakato wa kutuma maombi ya kuandaa Kombe la Dunia lakini akakanusha kuwa zilikuwa za rushwa. Alisema fedha hizo zilikuwa za maendeleo ya kandanda katika ukanda wa Karibea. Valke anasema hana hatia ya kuhusika na ufisadi katika malipo hayo na hivyo hatojiuzulu. Rais wa FIFA Sepp Blatter alijiuzulu siku nne baada ya kuchaguliwa.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters
Mhariri: Josephat Charo