SiasaHong Kong
Waratibu wa mkesha wa Tiananmen wahukumiwa kifungo
11 Machi 2023Matangazo
Watu hao wamehukumiwa kwa kushindwa kuipa mamlaka maelezo kuhusu muungano wao kulingana na sheria ya usalama wa kitaifa. Chow Hang-tung, Tang Ngok-kwan na Tsui Hon-kwong walikamatwa wakati wa msako huo wa mwaka 2021 kufuatia maandamano makubwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
Watatu hao walikuwa viongozi wa Muungano wa Hong Kong wa kuunga mkono harakati za demokrasia za kizalendo walipatikana na hatia wiki iliyopita. Chini ya utekelezaji wa sheria hiyo ya usalama, mkuu wa polisi anaweza kuomba habari tofauti kutoka kwa wakala wa kigeni. Kushindwa kuzingatia ombi hilo kunaweza kusababisha kifungo cha miezi sita jela na faini ya dola 12,740 iwapo utapatikana na hatia.