Warasaw:Uchaguzi wa bunge wa mapema Poland
21 Oktoba 2007Matangazo
Wapiga kura nchini Poland leo wanashiriki katika uchaguzi wa bunge ulioitishwa mapema baada ya kuvunjika serikali ya muungano. Waziri mkuu Jaroslaw Kaczynski kutoka chama cha kihafidhina cha sheria na haki, anakabiliwa na upinzani wa chama cha Jukawaa la kiraia kinachoongozwa na Donald Tusk. Uchaguzi huo umeitishwa miaka mitili kabla ya kipindi cha miaka minne kumalizika. Waziri mkuu Kaczynski ameitisha uchaguzi huo baada ya serikali yake ya mseto kuanguka kufuatia mabishano juu uchunguzi kuhusiana na madai ya rushwa.