1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani washikilia Syria lazima iondoke Lebanon

3 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZy

Beirut:

Viongozi wa upinzani nchini Lebanon wametoa wito wa kuondoka kwa wanajeshi wote 14,000 wa Syria walioko nchini humo. Taarifa iliotolewa baada ya mkutano wa wanasaiasa karibu 70 wa upinzani, pia imedai watumishi wote wa idara za upelelezi za Syria nchini Lebanon kuihama na maafisa wa usalama wa Lebanon wanaoungwa mkono na Syria wajiuzulu. Taarifa hiyo pia ilisema mazungumzo juu ya kuundwa serikali mpya, yanaweza tu kufanyika ikiwa Rais Emile Lahoud anayeungwa mkono na Syria atakubaliana na masharti hayo.Viongozi wa Marekani na Ulaya nao pia wameitaka Syria iondowe majeshi yake nchini Lebanon.