Wapinzani wakubali kuacha kuigomea serikali Sierra Leone
20 Oktoba 2023Mbali na hilo, serikali na serikali zilikubaliana pia juu ya kukomeshwa kufunguliwa kwa kesi mahakamani zinazochochewa kisiasa.
Pande hizo mbili zilifikia makubaliano hayo Jumatano jioni (Oktoba 18) baada ya upatanishi wa Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya ECOWAS kufuatia uchaguzi wenye mvutano mwezi Juni, ambao ulipingwa vikali na chama cha upinzani cha All People's Congress (APC).
Soma zaidi: Upinzani waapa kutoshiriki katika uongozi Sierra Leone
Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone aliyechaguliwa tena kwa muhula wa pili, anatarajiwa kutoa hotuba kwa taifa kuhusu umoja na mshikamano.
Kiongozi wa chama hicho cha upinzani APC, Samura Kamara, anakabiliwa na mashitaka ya ubadhirifu wa mali ya umma alipokuwa waziri wa mambo ya nje, tuhuma ambazo anadai zimechochewa kisiasa.