1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani waelekea kushinda uchaguzi wa rais nchini Senegal

25 Machi 2024

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha upinzani nchini Senegal Bassirou Diomaye Faye, anaelekea kushinda uchaguzi na ameshapongezwa na wagombea wengine kadhaa wa upinzani.

https://p.dw.com/p/4e6Mt
Senegal | Uchaguzi 2024
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha upinzani nchini Senegal Bassirou Diomaye Picha: SEYLLOU/AFP

Hata hivyo upande wa serikali ya mseto inayotawala umesema unao uhakika wa kufanyika uchaguzi wa duru ya pili. Mgombea wa upande serikali ya mseto ni waziri mkuu wa zamani Amadou Ba anayeungwa mkono na rais anaemaliza muda wake madarakani, Macky Sall.

Senegal: Faye akaribia ushindi katika uchaguzi wa rais

Uchaguzi huo umefanyika baada ya miezi kadhaa ya ghasia na mgogoro wa kisiasa. Televisheni ya serikali imeripoti kwamba asilimia 71 ya waliojiandikisha walishiriki katika zoezi la kupiga kura.

Wagombea 19 waliwania kiti cha rais katika uchaguzi huo na ikiwa hakuna ataepata zaidi ya asilimia 50 ya kura, itafanyika duru nyingine ya uchaguzi. Matokeo kamili ya duru hiyo ya kwanza yanatarajiwa kufahamika kesho Jumanne.