1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji wa itikadi kali wameuwa wanajeshi watano wa Mali

13 Septemba 2021

Wapiganaji wa itikadi kali wameuwa wanajeshi watano wa Mali, katika shambulizi lililofanyika jana Jumapili nchini humo.

https://p.dw.com/p/40FNJ
Symbolbild Mali Islamistischer Terrorismus
Picha: Baba Ahmed/AP/dpa/picture alliance

Katika taarifa yake jeshi la nchi hiyo limesema hadi sasa kundi lililohusika na shambulizi hilo bado halijafahamika lakini washambuliaji watatu pia waliuwawa.

Awali, ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, (Minusma) ulitangaza kushambuliwa kwa askari wake watatu na kiripuzi, kulikotokea katika mabi yake ya Kidal, huko kaskazini/mashariki mwa taifa hilo.

Tangu kuanza kutokea matukio ya mapinduzi na uasi wa wafuasi wenye itikadi kali kwa upande wa Kaskazini, 2012, Mali imejikuta ikitumbukia katika misukosuko ambayo imesababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha, ambapo wengi wa hao ni raia wa kawaida.