1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji 78 wa Kamanda Haftar waachiliwa huru Lipya

13 Mei 2021

Wafungwa 78 waliokuwa wanamgambo wa mbabe wa kivita wa Libya, Jenerali Khalifa Haftar, wameachiliwa huru kutoka jela ya Jedaida mjini Tripoli jioni ya jana.

https://p.dw.com/p/3tLHI
Libyen Konflikt l dem libyschen General Khalifa Haftar treue Kämpfer
Picha: Getty Images/AFP/A. Doma

Wafungwa 78 waliokuwa wanamgambo wa mbabe wa kivita wa Libya, Jenerali Khalifa Haftar, wameachiliwa huru kutoka jela ya Jedaida mjini Tripoli jioni ya jana.

Mnamo mwezi Aprili mwaka 2019, Haftar alianzisha mapigano ya kuutwaa mji mkuu, Tripoli, yaliyopelekea kuzaliwa kambi mbili zilizokuwa zikisaidiwa na mataifa ya kigeni, kabla ya kurejea nyuma mwaka mmoja baadaye.

Wafungwa hao waliachiliwa kupitia msamaha uliotangazwa na serikali na kusimamiwa na waziri wa sheria, ikiwa sehemu ya kusaka muafaka wa kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba. Kuachiliwa kwa wafungwa hao kumekuja katika wakati ambapo Waislamu duniani wakianza siku tatu za maadhimisho ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Libya imezama kwenye machafuko na umwagaji damu tangu kupinduliwa na kisha kuuawa kwa Muammar Gaddafi kwenye mapinduzi yaliyosaidiwa na Jumuiya ya Kujihami ya NATO mwaka 2011.