1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji 50,000 wa Tigray waachishwa shughuli za kijeshi

27 Julai 2023

Zaidi ya wapiganaji 50,000 wa Tigray wameachishwa kufanya shughuli za kijeshi chini ya mkataba wa amani na serikali ya shirikisho, uliofikisha mwisho vita vya miaka miwili kati yao na serikali kuu.

https://p.dw.com/p/4UT0x
Residents in Tigray region demonstrate to go back to their home
Picha: Million Hailesilassie/DW

Kulingana na televisheni ya eneo hilo Tigray TV, taarifa hiyo imetolewa na naibu mkuu wa serikali ya mpito ya jimbo hilo Jenrali Tadesse Worede, aliyekuwa mkuu wa jeshi la Tigray wakati wa mapigano hayo.

Vyombo vya habari vilivyo karibu na pande zote mbili vilitangaza kwamba hatua hiyo ya kuwaondoa wapiganaji katika shughuli za upiganaji ilianza mnamo Mei 26.

Soma zaidi: Marekani yasimamisha misaada ya chakula nchini Ethiopia

Kwa sasa mapigano yamesitishwa na majeshi ya Eritrea yaliyokuwa yameingia Tigray kuliunga mkono jeshi la Ethiopia, yameondoka kutoka kwenye jimbo hilo.