1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Wang Yi kuzuru Washington kuanzia Alhamisi

24 Oktoba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi atafanya ziara mjini Washington wiki hii itakayoifungulia mlango ziara ya rais wa China Xi Jinping.

https://p.dw.com/p/4XwPv
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang YiPicha: Sputnik/Mikhail Metzel/REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi atafanya ziara mjini Washington wiki hii itakayoifungulia mlango ziara ya rais wa China Xi Jinping inayolenga kupunguza msuguano kati ya dola hizo mbili zenye nguvu kubwa duniani.

Wang atazuru Washington kuanzia Alhamisi hadi Jumamosi huku kukiwa na mivutano kuhusu biashara, vita vya Ukraine, mashariki ya kati, Taiwan na vitendo vya China upande wa baharini karibu na Ufilipino.

Wang anakwenda Washington kufuatia ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken aliyoifanya mjini Beijing mnano mwezi Juni.