1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake wengi Tanzania watumia tumbaku

31 Mei 2021

Matumizi ya tumbaku Tanzania yametajwa kuongezeka maradufu miongoni mwa wanawake ikilinganishwa na wanaume, hatua ambayo inatajwa kuathiri kwa kiwango kikubwa afya za watoto hasa walio chini ya umri wa miaka mitano

https://p.dw.com/p/3uEUS
DW eco@africa - Malawi
Picha: DW

Kulingana na utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Serikali ya Tanzania, kiwango cha wanaotumia bidhaa za tumbaku kimeongezeka kutoka asilimia 2.9 mwaka 2012 hadi asilimia 3.2 mwaka 2018. Kwa kuwa kundi hili hutegemewa katika malezi ya watoto kwenye jamii, watoto kuwekwa  kwenye hatari kubwa kutokana kuvuta moshi wa bidhaa za tumbaku kutoka kwa mtumiaji.

Katika taifa hilo linalolitazama zao la tumbaku kuwa miongoni mwa mazao yanayotegemewa kibiashara na kiuchumi, takriban watu 600,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na kuvuta moshi wa sigara kwa kuwa karibu na wavutaji huku asilimia 28 kati yao ni watoto.
Wakati Tanzania ikishuhudia idadi hiyo ya vifo kwa watu wake zaidi ya asilimia 40 ya bajeti ya Wizara ya Afya inatumika kugharamia mzigo unaotokana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo mengi kati yake yanatokana na matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku.

Kwa mujibu wa utafiti huo, vijana waliowahi kutumia tumbaku ya aina yoyote ile katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wanawakilisha asilimia 9.7, hatua inayoifanya Wizara ya Afya kuona inalo jukumu la kuhamasisha kuacha kwa hiyari matumizi ya tumbaku.Amesema Waziri Gwajima.

Wakati Tanzania ikiwa na jukumu la lazima kidunia kudhibiti matumizi ya tumbaku ili kufikia lengo la kutokomeza kabisa, wadau wanasema itahitaji utashi wa kisiasa ili kufikia lengo hilo kwani zao hilo linategemewa katika kuchangia pato la Taifa hilo lililoingia uchumi wa kati kiwango cha chini.

Simbabwe Kinder mit Tabak-Ballen
Watumiaji tumbaku Tanzania wameongezeka kutoka asilimia 2.9 mwaka 2012 hadi asilimia 3.2 mwaka 2018Picha: picture-alliance/AP Photo/T. Mukwazhi

Hawa Bihoga DW Dar es Salaam